Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 14:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Wapumbavu hujisemea moyoni:“Hakuna Mungu.”Wote wamepotoka kabisa,wametenda mambo ya kuchukiza;hakuna hata mmoja atendaye jema!

2. Mwenyezi-Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni,aone kama kuna yeyote mwenye busara,kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu.

3. Lakini wote wamekosa,wote wamepotoka pamoja;hakuna atendaye mema,hakuna hata mmoja.

4. “Je, hao watendao maovu hawana akili?Wanawatafuna watu wangu kama mikate;wala hawanijali mimi Mwenyezi-Mungu.”

5. Hapo watashikwa na hofu kubwa,maana Mungu yu pamoja na waadilifu.

6. Unaweza kuvuruga mipango ya maskini,lakini Mwenyezi-Mungu ndiye kimbilio lake.

7. Laiti ukombozi wa Israeli ungefika kutoka Siyoni!Mwenyezi-Mungu atakaporekebisha hali ya watu wake,wazawa wa Yakobo watashangilia;Waisraeli watafurahi.

Kusoma sura kamili Zaburi 14