3. Uniangalie na kunijibu, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu.Uyaangazie macho yangu, nisipatwe na usingizi wa kifo.
4. Usiwaache maadui zangu waseme: “Tumemweza huyu!”Watesi wangu wasije wakafurahia kuanguka kwangu.
5. Lakini mimi nazitumainia fadhili zako;moyo wangu na ufurahie wokovu wako.
6. Nitakuimbia wewe, ee Mwenyezi-Mungu,kwa ukarimu mwingi ulionitendea!