4. Wao husema: “Kwa ndimi zetu tutashinda;midomo tunayo, nani awezaye kututawala?”
5. Lakini Mwenyezi-Mungu asema:“Kwa sababu maskini wanadhulumiwa,na wahitaji wanapiga kite, sasa naja,nami nitawapa usalama wanaoutazamia.”
6. Neno la Mwenyezi-Mungu ni safi,safi kama fedha iliyosafishwa katika tanuri,naam, kama fedha iliyosafishwa mara saba.
7. Utulinde, ee Mwenyezi-Mungu,utukinge daima na kizazi hiki kiovu.
8. Waovu wanazunguka kila mahali;upotovu unatukuzwa kati ya watu.