3. Mwovu hujisifia tamaa zake mbaya,mtu wa tamaa hulaani na kumkataa Mwenyezi-Mungu.
4. Katika majivuno yake husema: “Mungu hatagundua.”Mawazo yake yote ni: “Hakuna Mungu.”
5. Njia za mwovu hufanikiwa daima;kwake hukumu zako ziko mbali na mawazo yake,na huwadharau maadui zake wote.
6. Huwaza moyoni: “Sitakuwa na wasiwasi;sitapatwa na dhiki maishani.”
7. Kinywa chake kimejaa laana, udanganyifu na dhuluma;mwepesi kusema maneno ya kuchukiza na maovu.
8. Hujificha vijijini huku anaotea,amuue kwa siri mtu asiye na hatia.Yuko macho kumvizia mnyonge;
9. huotea mafichoni mwake kama simba.Huvizia apate kuwakamata maskini;huwanasa kwa mtego wake na kuwachukua.
10. Mnyonge huvamiwa na kuangushwa chini;huangushwa kwa ukatili wa mtu mwovu.