13. Ee Mungu, kwa nini mwovu anakudharau,na kusema ati hutamfanya awajibike?
14. Lakini wewe wawaona wenye dhiki na shida;nawe daima uko tayari kuwasaidia.Mnyonge anakutegemea wewe, ee Mungu,wewe umekuwa daima msaada wa yatima.
15. Uzivunje nguvu za mtu mwovu;ukomeshe uovu wake wote, usiwepo tena.
16. Mwenyezi-Mungu ni mfalme milele na milele!Mataifa yasiyomjua yatatoweka nchini mwake.
17. Ee Mwenyezi-Mungu, wapokea dua za mnyonge;wampa moyo na kumtegea sikio.
18. Utawatendea haki yatima na wanaodhulumiwa,binadamu aliye udongo asiweze tena kuleta hofu.