Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 10:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ee Mwenyezi-Mungu, mbona wasimama mbali?Kwa nini wajificha wakati tumo taabuni?

2. Kwa kiburi waovu wanawatesa maskini;njama zao ziwanase wao wenyewe.

3. Mwovu hujisifia tamaa zake mbaya,mtu wa tamaa hulaani na kumkataa Mwenyezi-Mungu.

4. Katika majivuno yake husema: “Mungu hatagundua.”Mawazo yake yote ni: “Hakuna Mungu.”

5. Njia za mwovu hufanikiwa daima;kwake hukumu zako ziko mbali na mawazo yake,na huwadharau maadui zake wote.

6. Huwaza moyoni: “Sitakuwa na wasiwasi;sitapatwa na dhiki maishani.”

7. Kinywa chake kimejaa laana, udanganyifu na dhuluma;mwepesi kusema maneno ya kuchukiza na maovu.

8. Hujificha vijijini huku anaotea,amuue kwa siri mtu asiye na hatia.Yuko macho kumvizia mnyonge;

9. huotea mafichoni mwake kama simba.Huvizia apate kuwakamata maskini;huwanasa kwa mtego wake na kuwachukua.

10. Mnyonge huvamiwa na kuangushwa chini;huangushwa kwa ukatili wa mtu mwovu.

Kusoma sura kamili Zaburi 10