Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 6:23-26 Biblia Habari Njema (BHN)

23. Basi, wale vijana wapelelezi wakaenda; wakamleta Rahabu, baba yake na mama yake, ndugu zake na watu wote wa jamaa yake, wakawaweka nje ya kambi ya Israeli.

24. Kisha, wakauchoma moto mji wa Yeriko na kila kitu kilichokuwako isipokuwa fedha, dhahabu, vyombo vya shaba na vya chuma; hivyo viliwekwa katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

25. Lakini yule kahaba Rahabu pamoja na watu wote wa nyumba ya baba yake, Yoshua aliyaokoa maisha yao. Rahabu akaishi miongoni mwa Waisraeli hadi leo, kwa kuwa aliwaficha wajumbe ambao Yoshua aliwatuma kwenda kuupeleleza mji wa Yeriko.

26. Wakati huo Yoshua alitamka apizo rasmi mbele ya watu akisema,“Atakayeujenga tena mji wa Yeriko,na alaaniwe na Mungu,Yeyote atakayeweka msingi wa mji huo,mzaliwa wake wa kwanza na afe.Yeyote atakayejenga lango la mji huo,mwanawe kitinda mimba na afe.”

Kusoma sura kamili Yoshua 6