Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 21:5-24 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Watu wa ukoo wa Kohathi waliosalia walipewa miji kumi iliyoko katika maeneo ya makabila ya Efraimu, Dani na katika eneo la nusu ya kabila la Manase.

6. Watu wa ukoo wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu katika maeneo ya makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na katika eneo la nusu ya kabila la Manase huko Bashani.

7. Jamaa za ukoo wa Merari walipewa miji kumi na miwili katika maeneo ya makabila ya Reubeni, Gadi na Zebuluni.

8. Waisraeli waliwapa Walawi miji hiyo pamoja na vijiji vya malisho yao, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza Mose.

9. Yafuatayo ni majina ya miji kutoka kwenye maeneo ya kabila la Yuda na Simeoni ambayo ilitolewa kwa

10. wazawa wa kuhani Aroni, waliokuwa jamaa za ukoo wa Kohathi ambaye alikuwa wa kabila la Lawi. Sehemu yao walipata kwanza kwani kura yao ilitokea kwanza.

11. Walipewa Kiriath-arba yaani Hebroni (Arba alikuwa baba yake Anaki) katika milima ya Yuda, pamoja na mbuga zilizoizunguka.

12. Lakini mashamba ya mji huo pamoja na vijiji vilivyouzunguka alikuwa amekwisha pewa Kalebu mwana wa Yefune viwe mali yake.

13. Licha ya kuwapa wazawa wa kuhani Aroni mji wa Hebroni ambao pia ulikuwa umetengwa kuwa mji wa kukimbilia usalama, waliwapa miji ya Libna pamoja na mbuga zake za malisho,

14. Yatiri pamoja na mbuga zake za malisho, Eshtemoa pamoja na mbuga zake za malisho,

15. Holoni pamoja na mbuga zake za malisho, Debiri pamoja na mbuga zake za malisho,

16. Aini pamoja na mbuga zake za malisho, Yuta pamoja na mbuga zake za malisho na Beth-shemeshi pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji hiyo iliyo katika maeneo ya makabila hayo mawili ni tisa.

17. Katika eneo la kabila la Benyamini walipewa miji mingine: Gibeoni pamoja na mbuga zake za malisho,

18. Anathothi pamoja na mbuga zake za malisho, Almoni pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni minne.

19. Miji yote ya wazawa wa Aroni ambao walikuwa makuhani, ilikuwa kumi na mitatu pamoja na mbuga zao za malisho.

20. Watu waliosalia wa ukoo wa Kohathi, ambao pia ni jamaa za kabila la Lawi walipewa miji katika eneo la kabila la Efraimu.

21. Walipewa Shekemu, mji ambao ulikuwa pia mji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho katika nchi ya milima ya Efraimu, na Gezeri pamoja na mbuga zake za malisho,

22. Kibzaimu pamoja na mbuga zake za malisho na Beth-horoni pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni minne.

23. Katika eneo la kabila la Dani walipewa Elteke pamoja na mbuga zake za malisho, Gibethoni pamoja na mbuga zake za malisho,

24. Aiyaloni pamoja na mbuga zake za malisho na Gath-rimoni pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni minne.

Kusoma sura kamili Yoshua 21