Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 19:34-46 Biblia Habari Njema (BHN)

34. Kutoka hapo mpaka ulikwenda magharibi kuelekea Aznoth-tabori; toka huko ukaenda Hukoki na kugusana na pembe ya kusini ya eneo la kabila la Zebuluni; kisha kugusana na eneo la kabila la Asheri upande wa magharibi, na kugusana na eneo la kabila la Yuda. Kwa upande wa mashariki mpaka ukiingilia kwenye mto Yordani.

35. Miji yao iliyokuwa na ngome ni Zidimu, Zeri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi,

36. Adama, Rama, Hazori,

37. Kedeshi, Edrei, En-hazori,

38. Yironi, Migdaleli, Horemu, Beth-anathi na Beth-shemeshi. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na tisa pamoja na vijiji vyake.

39. Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Naftali; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

40. Kura ya saba ilizipata koo za kabila la Dani.

41. Eneo la nchi yao lilikuwa na miji ya Sora, Eshtaoli, Ir-shemeshi

42. Shaalabini, Aiyaloni, Yithla,

43. Eloni, Timna, Ekroni

44. Elteke, Gibethoni, Baalathi,

45. Yehudi, Bene-beraki, Gath-rimoni,

46. Me-yarkoni na Rakoni na nchi iliyokuwa karibu na Yopa.

Kusoma sura kamili Yoshua 19