1. Basi, Yona, akiwa tumboni mwa samaki huyo, akawa akimwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wake,
2. akisema:“Kwa sababu ya taabu yangu,nilikuomba, ee Mwenyezi-Mungu,nawe ukanisikiliza;toka chini kuzimu, nilikulilia,nawe ukasikiliza kilio changu.
3. Ulinitupa katika kilindi, katikati ya bahari,gharika ikanizunguka,mawimbi na gharika vikapita juu yangu.