Agano la Kale

Agano Jipya

Yoeli 2:6-13 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Wakaribiapo, watu hujaa hofu,nyuso zao zinawaiva.

7. Wanashambulia kama mashujaa wa vita;kuta wanazipanda kama wanajeshi.Wote wanakwenda mbele moja kwa moja,bila hata mmoja wao kubadilisha njia.

8. Hakuna amsukumaye mwenziwe;kila mmoja anafuata mkondo wake.Wanapita kati ya vizuizi vya silaha,wala hakuna kiwezacho kuwazuia.

9. Wanauvamia mji,wanapiga mbio ukutani;wanaziparamia nyumba na kuingia,wanapenya madirishani kama wezi.

10. Nchi inatetemeka mbele yao,mbingu zinatikisika.Jua na mwezi vyatiwa giza,nazo nyota zinaacha kuangaza.

11. Mwenyezi-Mungu anaamuru jeshi lake kwa sauti;askari wake ni wengi mno,wanaomtii hawahesabiki.2Siku ya Mwenyezi-Mungu kweli ni kuu na ya kutisha sana!Nani atakayeweza kuistahimili?

12. “Lakini hata sasa,”nasema mimi Mwenyezi-Mungu,“Nirudieni kwa moyo wote,kwa kufunga, kulia na kuomboleza.

13. Msirarue mavazi yenu kuonesha huzunibali nirudieni kwa moyo wa toba.”Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu;yeye amejaa neema na huruma;hakasiriki upesi, ni mwingi wa fadhili;daima yu tayari kuacha kuadhibu.

Kusoma sura kamili Yoeli 2