Agano la Kale

Agano Jipya

Yoeli 2:22-32 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Msiogope, enyi wanyama.malisho ya nyikani yamekuwa mazuri,miti inazaa matunda yake,mizabibu na mitini zinazaa kwa wingi.

23. “Furahini, enyi watu wa Siyoni,shangilieni kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,maana amewapeni mvua za masika,amewapeni mvua ya kutosha:Mvua za masika na mvua za vuli kama hapo awali.

24. Mahali pa kupuria patajaa nafaka,mashinikizo yatafurika divai na mafuta.

25. Nitawarudishia miaka ile iliyoliwa na nzige,kila kitu kilicholiwa na tunutu, parare na matumatu,hilo jeshi kubwa nililowaletea!

26. Mtapata chakula kingi na kutosheka;mtalisifu jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,aliyewatendea mambo ya ajabu.Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.

27. Mtatambua kwamba mimi nimo miongoni mwenu,enyi Waisraeli;kwamba mimi Mwenyezi-Mungu,ndimi Mungu wenu wala hakuna mwingine.Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.

28. “Kisha hapo baadayenitaimimina roho yangu juu ya binadamu wote.Watoto wenu wa kike na wa kiume watatabiri,wazee wenu wataota ndoto,na vijana wenu wataona maono.

29. Hata juu ya watumishi wa kiume na wa kike,nitaimimina roho yangu wakati huo.

30. “Nitatoa ishara mbinguni na duniani;kutakuwa na damu, moto na minara ya moshi.

31. Jua litatiwa giza,na mwezi utakuwa mwekundu kama damu,kabla ya kufika siku ya Mwenyezi-Mungu,siku iliyo kuu na ya kutisha.

32. Hapo watu wote watakaoomba kwa jina la Mwenyezi-Mungu wataokolewa.Maana katika mlima Siyoni na Yerusalemu,watakuwako watu watakaosalimika,kama nilivyosema mimi Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Yoeli 2