Agano la Kale

Agano Jipya

Yoeli 2:15-23 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Pigeni tarumbeta huko Siyoni!Toeni amri watu wafunge;itisheni mkutano wa kidini.

16. Wakusanyeni watu wote,wawekeni watu wakfu.Waleteni wazee,wakusanyeni watoto,hata watoto wanyonyao.Bwana arusi na bibi arusina watoke vyumbani mwao.

17. Kati ya madhabahu na lango la hekalu,makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu,walie na kuomba wakisema:“Wahurumie watu wako, ee Mwenyezi-Mungu.Usiyaache mataifa mengine yatudharauna kutudhihaki yakisema,‘Yuko wapi basi Mungu wao?’”

18. Ndipo Mwenyezi-Mungu akaipenda nchi yakeakawahurumia watu wake.

19. Alisikiliza, akajibu sala zao; akasema,“Sasa nitawapeni tena nafaka,sitawafanya mdharauliwe tena na mataifa.

20. Nitawaondoa hao adui watokao kaskazini,nitawafukuza mpaka jangwani;askari wa mbele nitawatupa katika Bahari ya Chumvina wale wa nyuma katika Bahari ya Mediteranea.Watatoa uvundo na harufu mbaya,hao ambao wamefanya maovu makubwa.

21. “Usiogope, ewe nchi,bali furahi na kushangilia,maana Mwenyezi-Mungu ametenda makuu.

22. Msiogope, enyi wanyama.malisho ya nyikani yamekuwa mazuri,miti inazaa matunda yake,mizabibu na mitini zinazaa kwa wingi.

23. “Furahini, enyi watu wa Siyoni,shangilieni kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,maana amewapeni mvua za masika,amewapeni mvua ya kutosha:Mvua za masika na mvua za vuli kama hapo awali.

Kusoma sura kamili Yoeli 2