Agano la Kale

Agano Jipya

Yoeli 2:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Pigeni tarumbeta huko Siyoni;pigeni baragumu juu ya mlima mtakatifu!Tetemekeni enyi wakazi wa Yuda,maana siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja,naam, siku hiyo iko karibu!

2. Hiyo ni siku ya giza na huzuni;siku ya mawingu na giza nene.Jeshi kubwa la nzige linakaribiakama giza linalotanda milimani.Namna hiyo haijapata kuweko kamwewala haitaonekana tenakatika vizazi vyote vijavyo.

3. Kama vile moto uteketezavyojeshi hilo laharibu kila kitu mbele yakena kuacha nyuma kila kitu kinateketezwa;kabla hawajapita, nchi ni kama bustani ya Edeni,lakini wakisha pita, ni jangwa tupu.Hakuna kiwezacho kuwaepa!

4. Wanaonekana kama farasi,wanashambulia kama farasi wa vita,

5. Wanaporukaruka kwenye vilele vya milima,wanarindima kama magari ya farasi,wanavuma kama mabua makavu motoni.Wamejipanga kama jeshi kubwatayari kabisa kufanya vita.

6. Wakaribiapo, watu hujaa hofu,nyuso zao zinawaiva.

Kusoma sura kamili Yoeli 2