Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 7:17-21 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Binadamu ni nini hata umjali?Kwa nini hata unajishughulisha naye?

18. Wewe waja kumchunguza kila asubuhi,kila wakati wafika kumjaribu!

19. Utaendelea kuniangalia hata lini,bila kuniacha hata nimeze mate?

20. Kama nikitenda dhambi,yakudhuru nini ewe mkaguzi wa binadamu?Mbona umeniweka kuwa shabaha ya mapigo yako?Je, mimi nimekuwa mzigo kwako?

21. Mbona hunisamehi kosa languna kuniondolea uovu wangu?Hivi punde nitalazwa chini kaburini,utanitafuta, lakini sitakuwapo tena!”

Kusoma sura kamili Yobu 7