Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 7:10-19 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Anayeondoka harudi tena kwa jamaa yake,na pale alipokuwa anaishi husahaulika mara.

11. “Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu kuongea;nitasema kwa msongo wa roho yangu,nitalalamika kwa uchungu wa nafsi yangu.

12. Je, mimi ni bahari au dude la baharinihata uniwekee mlinzi?

13. Nikisema, ‘Kitanda kitanipumzisha,malazi yangu yatanipunguzia malalamiko yangu,’

14. wewe waja kunitia hofu kwa ndoto,wanitisha kwa kuniletea maono;

15. hata naona afadhali kujinyonga,naona heri kufa kuliko kupata mateso haya.

16. Nayachukia maisha yangu;sitaishi milele.Niacheni, maana siku zangu ni pumzi tu!

17. Binadamu ni nini hata umjali?Kwa nini hata unajishughulisha naye?

18. Wewe waja kumchunguza kila asubuhi,kila wakati wafika kumjaribu!

19. Utaendelea kuniangalia hata lini,bila kuniacha hata nimeze mate?

Kusoma sura kamili Yobu 7