Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 41:9-20 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Yameunganishwa pamoja,hata haiwezekani kuyatenganisha.

10. Likipiga chafya, mwanga huchomoza,macho yake humetameta kama jua lichomozapo.

11. Kinywani mwake hutoka mienge iwakayo,cheche za moto huruka nje.

12. Puani mwake hufuka moshi,kama vile chungu kinachochemka;kama vile magugu yawakayo.

13. Pumzi yake huwasha makaa;mwali wa moto hutoka kinywani mwake.

14. Shingo yake ina nguvu ajabu,litokeapo watu hukumbwa na hofu.

15. Misuli yake imeshikamana pamoja,imara kama chuma wala haitikisiki.

16. Moyo wake ni mgumu kama jiwe,mgumu kama jiwe la kusagia.

17. Linapoinuka, mashujaa hushikwa na woga,kwa pigo moja huwa wamezirai.

18. Hakuna upanga uwezao kulijeruhi,wala mkuki, mshale au fumo.

19. Kwake chuma ni laini kama unyasi,na shaba kama mti uliooza.

20. Mshale hauwezi kulifanya likimbie;akitupiwa mawe ya teo huyaona kama makapi.

Kusoma sura kamili Yobu 41