Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 41:18-25 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Hakuna upanga uwezao kulijeruhi,wala mkuki, mshale au fumo.

19. Kwake chuma ni laini kama unyasi,na shaba kama mti uliooza.

20. Mshale hauwezi kulifanya likimbie;akitupiwa mawe ya teo huyaona kama makapi.

21. Kwake, rungu ni kama kipande cha bua,hucheka likitupiwa fumo kwa wingi.

22. Tumbo lake ni kama limefunikwa na vigae vikali;hukwaruza na kurarua udongo kama chombo cha kupuria.

23. Bahari huisukasuka kama maji yachemkayo,huifanya itoe povu kama chupa ya mafuta.

24. Lipitapo huacha nyuma alama inayongaa;povu jeupe huonekana limeelea baharini.

25. Duniani hakuna kinachofanana nalo;hilo ni kiumbe kisicho na hofu.

Kusoma sura kamili Yobu 41