Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 38:5-17 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Ni nani aliyeweka vipimo vyake, wajua bila shaka!Au nani aliyelaza kamba juu yake kuipima?

6. Je, nguzo za dunia zimesimikwa juu ya nini,au nani aliyeliweka jiwe lake la msingi,

7. nyota za asubuhi zilipokuwa zikiimba pamoja,na wana wa Mungu wakapaza sauti za shangwe?

8. Ni nani aliyeyafunga mafuriko ya bahariwakati yalipozuka na kuvuma kutoka vilindini?

9. Mimi ndiye niliyeifunika bahari kwa mawinguna kuiviringishia giza nene.

10. Niliiwekea bahari mipaka,nikaizuia kwa makomeo na milango,

11. nikaiambia: ‘Mwisho wako ni hapa, si zaidi!Mawimbi yako ya nguvu yatakomea hapa!’

12. “Yobu, tangu uzaliwe umewahi kuamuru kupambazuke?na kulifanya pambazuko lijue mahali pake,

13. ili lipate kuikamata dunia kwa pembe zakena kuwatimulia mbali waovu waliomo?

14. Dunia hugeuka na kupata rangi kama vazi;kama udongo wa mfinyanzi unavyogeuzwa na mhuri.

15. Lakini waovu watanyimwa mwanga wao,mkono wanaonyosha kupiga watu utavunjwa.

16. “Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari?au kutembea juu ya sakafu ya kilindi cha bahari?

17. Je, umewahi kuoneshwa malango ya kifo,au kuyaona malango ya makazi ya giza nene?

Kusoma sura kamili Yobu 38