Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 38:36-41 Biblia Habari Njema (BHN)

36. Ni nani aliyemjulisha kwarara kujaa kwa mto Niliau aliyemwambia jogoo kwamba mvua inakuja?

37. Nani mwenye akili ya kuweza kuhesabu mawingu,au kuinamisha viriba vya maji huko mbinguni?

38. ili vumbi duniani igandamanena udongo ushikamane na kuwa matope?

39. “Je, waweza kumwindia simba mawindo yakeau kuishibisha hamu ya wana simba;

40. wanapojificha mapangoni mwao,au kulala mafichoni wakiotea?

41. Ni nani awapaye kunguru chakula chao,makinda yao yanaponililia mimi Mungu,na kurukaruka huku na huko kwa njaa?

Kusoma sura kamili Yobu 38