Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 38:25-38 Biblia Habari Njema (BHN)

25. “Nani aliyechora angani njia kwa ajili ya mvua?Nani aliyeionesha radi njia yake mawinguni,

26. ikasababisha mvua kunyesha nchini kusikoishi mtuna jangwani ambako hakuna mtu,

27. ili kuiburudisha nchi kavu na kamena kuifanya iote nyasi?

28. “Je, mvua ina baba?Au nani ameyazaa matone ya umande?

29. Je, barafu ilitoka tumboni kwa nani?Nani aliyeizaa theluji?

30. Maji hugeuka kuwa magumu kama jiwe,na uso wa bahari ukaganda.

31. “Angalia makundi ya nyota:Je, unaweza kuifunga minyororo Kilimia,au kuvilegeza vifungo vya Orioni?

32. Je, waweza kuziongoza nyota katika majira yake,au kumwongoza Dubu pamoja na watoto wake?

33. Je, wazijua kanuni zinazotawala mbingu;Je, waweza kuzipangia taratibu zao duniani?

34. “Je, waweza kupaza sauti na kuyaamuru mawinguyakufunike kwa mtiririko wa mvua?

35. Je, wewe ukiamuru umeme umulike,utakujia na kusema: ‘Nipo hapa?’

36. Ni nani aliyemjulisha kwarara kujaa kwa mto Niliau aliyemwambia jogoo kwamba mvua inakuja?

37. Nani mwenye akili ya kuweza kuhesabu mawingu,au kuinamisha viriba vya maji huko mbinguni?

38. ili vumbi duniani igandamanena udongo ushikamane na kuwa matope?

Kusoma sura kamili Yobu 38