Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 38:18-34 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Je, wajua ukubwa wa dunia?Niambie kama unajua haya yote.

19. “Je, makao ya mwanga yako wapi?Nyumbani kwa giza ni wapi,

20. ili upate kulipeleka kwenye makao yake,na kuifahamu njia ya kwenda huko kwake.

21. Wewe unapaswa kujua,wewe ambaye umekwisha ishi miaka mingi!

22. “Je, umewahi kuingia katika bohari za theluji,au kuona bohari za mvua ya mawe

23. ambavyo nimevihifadhi kwa ajili ya wakati wa fujo,kwa ajili ya siku ya mapigano na vita?

24. Ipi njia ya kwenda mahali mwanga unapogawanywa,au huko kunakotoka upepo wa mashariki ukasambazwa duniani?

25. “Nani aliyechora angani njia kwa ajili ya mvua?Nani aliyeionesha radi njia yake mawinguni,

26. ikasababisha mvua kunyesha nchini kusikoishi mtuna jangwani ambako hakuna mtu,

27. ili kuiburudisha nchi kavu na kamena kuifanya iote nyasi?

28. “Je, mvua ina baba?Au nani ameyazaa matone ya umande?

29. Je, barafu ilitoka tumboni kwa nani?Nani aliyeizaa theluji?

30. Maji hugeuka kuwa magumu kama jiwe,na uso wa bahari ukaganda.

31. “Angalia makundi ya nyota:Je, unaweza kuifunga minyororo Kilimia,au kuvilegeza vifungo vya Orioni?

32. Je, waweza kuziongoza nyota katika majira yake,au kumwongoza Dubu pamoja na watoto wake?

33. Je, wazijua kanuni zinazotawala mbingu;Je, waweza kuzipangia taratibu zao duniani?

34. “Je, waweza kupaza sauti na kuyaamuru mawinguyakufunike kwa mtiririko wa mvua?

Kusoma sura kamili Yobu 38