Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 38:12-20 Biblia Habari Njema (BHN)

12. “Yobu, tangu uzaliwe umewahi kuamuru kupambazuke?na kulifanya pambazuko lijue mahali pake,

13. ili lipate kuikamata dunia kwa pembe zakena kuwatimulia mbali waovu waliomo?

14. Dunia hugeuka na kupata rangi kama vazi;kama udongo wa mfinyanzi unavyogeuzwa na mhuri.

15. Lakini waovu watanyimwa mwanga wao,mkono wanaonyosha kupiga watu utavunjwa.

16. “Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari?au kutembea juu ya sakafu ya kilindi cha bahari?

17. Je, umewahi kuoneshwa malango ya kifo,au kuyaona malango ya makazi ya giza nene?

18. Je, wajua ukubwa wa dunia?Niambie kama unajua haya yote.

19. “Je, makao ya mwanga yako wapi?Nyumbani kwa giza ni wapi,

20. ili upate kulipeleka kwenye makao yake,na kuifahamu njia ya kwenda huko kwake.

Kusoma sura kamili Yobu 38