Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 38:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hapo Mwenyezi-Mungu alimjibu Yobu kutoka dhoruba:

2. “Nani wewe unayevuruga mashauri yangukwa maneno yasiyo na akili?

3. Jikaze kama mwanamume,nami nitakuuliza nawe utanijibu.

4. “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia?Niambie, kama una maarifa.

5. Ni nani aliyeweka vipimo vyake, wajua bila shaka!Au nani aliyelaza kamba juu yake kuipima?

6. Je, nguzo za dunia zimesimikwa juu ya nini,au nani aliyeliweka jiwe lake la msingi,

7. nyota za asubuhi zilipokuwa zikiimba pamoja,na wana wa Mungu wakapaza sauti za shangwe?

8. Ni nani aliyeyafunga mafuriko ya bahariwakati yalipozuka na kuvuma kutoka vilindini?

9. Mimi ndiye niliyeifunika bahari kwa mawinguna kuiviringishia giza nene.

Kusoma sura kamili Yobu 38