Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 31:4-20 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Je, Mungu haoni njia zangu,na kujua hatua zangu zote?

5. “Kama nimeishi kwa kufuata uongo,kama nimekuwa mbioni kudanganya watu,

6. Mungu na anipime katika mizani ya haki,naye ataona kwamba sina hatia.

7. Kama hatua zangu zimepotoka,moyo wangu ukafuata tamaa za macho yangu;kama mikono yangu imechafuliwa na dhambi,

8. jasho langu na liliwe na mtu mwingine,mazao yangu shambani na yangolewe.

9. “Kama moyo wangu umevutwa kwa mke wa mtu,kama nimenyemelea mlangoni kwa jirani yangu,

10. basi, mke wangu na ampikie mume mwingine,na wanaume wengine wamtumie.

11. Jambo hilo ni kosa kuu la jinai,uovu ambao hakimu lazima atoe adhabu.

12. Kosa langu lingekuwa kama moto,wa kuniteketeza na kuangamiza,na kuchoma kabisa mapato yangu yote.

13. Kama nimekataa kesi ya mtumishi wanguwa kiume au wa kike,waliponiletea malalamiko yao,

14. nitafanya nini basi Mungu atakaponikabili?Je, akinichunguza nitamjibu nini?

15. Maana Mungu ndiye aliyeniumba mimi na mtumishi wangu;yeye ndiye aliyetuumba sisi wote.

16. “Je, nimepata kumnyima maskini mahitaji yakeau kuwafanya wajane watumaini bure?

17. Je, nimekula chakula changu peke yangu,bila kuwaachia yatima nao wapate chochote?

18. La! Tangu ujana wangu nimekuwa mlezi wao,tangu utoto wangu nimewaongoza wajane.

19. Je, nilimwona mtu anakufa kwa kukosa nguo,au maskini ambaye hana nguo ya kuvaa,

20. bila kumpa joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo wangunaye akanitakia baraka za shukrani ya moyo?

Kusoma sura kamili Yobu 31