Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 31:23-40 Biblia Habari Njema (BHN)

23. Maana maafa kutoka kwa Mungu ni kitisho kwangu;mimi siwezi kuukabili ukuu wake.

24. “Je, tumaini langu nimeliweka katika dhahabu,au, nimeiambia dhahabu safi, ‘Wewe ni usalama wangu?’

25. Je, nimepata kufurahia wingi wa utajiri wanguau kujivunia mapato ya mikono yangu?

26. Kama nimeliangalia jua likiangaza,na mwezi ukipita katika uzuri wake,

27. na moyo wangu ukashawishika kuviabudu,nami nikaibusu mikono yangu kwa heshima yake,

28. huo pia ungekuwa uovu wa kuadhibiwa na mahakimumaana ningekuwa mwongo mbele ya Mungu aliye juu.

29. “Je, nimefurahia kuangamia kwa adui yangu,au kufurahi alipopatwa na maafa?

30. La! Sikuruhusu kinywa changu kumtakia mabaya,kwa kumlaani ili afe.

31. Watumishi wangu wote wanasema wazikila mgeni amekaribishwa nyumbani mwangu.

32. Msafiri hakulala nje ya nyumba yangu,nilimfungulia mlango mpita njia.

33. Je nimeficha makosa yangu kama wengine?Je nimekataa kukiri dhambi zangu?

34. Sijaogopa kusimama mbele ya umati wa watu,wala kukaa kimya au kujifungia ndani,eti kwa kuogopa kutishwa na dharau zao.

35. Laiti angekuwapo mtu wa kunisikiliza!Naweza kutia sahihi yangu katika kila nilichosema.Namwambia Mungu Mwenye Nguvu anijibu!Laiti mashtaka wanayonitolea maadui zangu yangeandikwa!

36. Ningeyavaa kwa maringo mabeganina kujivisha kichwani kama taji.

37. Ningemhesabia Mungu kila kitu nilichofanya,ningemwendea kama mwana wa mfalme.

38. Kama nimeiiba ardhi ninayoilima,nikasababisha mifereji yake iomboleze,

39. kwa kufaidika na mazao yake bila kulipana kusababisha kifo cha wenyewe,

40. basi miiba na iote humo badala ya ngano,na magugu badala ya shayiri.”Mwisho wa hoja za Yobu.

Kusoma sura kamili Yobu 31