Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 3:8-17 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Walozi wa siku waulaani,watu stadi wa kuligutua dude Lewiyathani waulaani!

9. Nyota zake za pambazuko zififie,utamani kupata mwanga, lakini usipate,wala usione nuru ya pambazuko.

10. Maana usiku huo haukulifunga tumbo la mama,wala kuficha taabu nisizione.

11. Mbona sikufa nilipozaliwa,nikatoka tumboni na kutoweka?

12. Kwa nini mama yangu alinizaa?Kwa nini nikapata kunyonya?

13. Maana ningekuwa nimezikwa, kimya;ningekuwa nimelazwa na kupumzika,

14. pamoja na wafalme na watawala wa dunia,waliojijengea upya magofu yao;

15. ningekuwa pamoja na wakuu waliokuwa na dhahabu,waliojaza nyumba zao fedha tele.

16. Au, mbona sikuwa kama mimba iliyoharibika,naam, kama mtoto aliyezaliwa mfu?

17. Huko kwa wafu waovu hawamsumbui mtu,huko wachovu hupumzika.

Kusoma sura kamili Yobu 3