Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 3:21-26 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Mtu atamaniye kifo lakini hafi;hutafuta kifo kuliko hazina iliyofichika.

22. Mtu kama huyo atashangilia mno na kufurahi,atafurahi atakapokufa na kuzikwa!

23. Ya nini kumjalia uhai mtu ambaye njia zake zimefungwa,mtu ambaye Mungu amemwekea kizuizi?

24. Kwa maana kusononeka ndio mkate wangu,kupiga kite kwangu kunatiririka mithili ya maji.

25. Kile ninachokiogopa kimenipata,ninachokihofia ndicho kilichonikumba.

26. Sina amani wala utulivu;sipumziki, taabu imenijia.”

Kusoma sura kamili Yobu 3