Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 3:11-24 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Mbona sikufa nilipozaliwa,nikatoka tumboni na kutoweka?

12. Kwa nini mama yangu alinizaa?Kwa nini nikapata kunyonya?

13. Maana ningekuwa nimezikwa, kimya;ningekuwa nimelazwa na kupumzika,

14. pamoja na wafalme na watawala wa dunia,waliojijengea upya magofu yao;

15. ningekuwa pamoja na wakuu waliokuwa na dhahabu,waliojaza nyumba zao fedha tele.

16. Au, mbona sikuwa kama mimba iliyoharibika,naam, kama mtoto aliyezaliwa mfu?

17. Huko kwa wafu waovu hawamsumbui mtu,huko wachovu hupumzika.

18. Huko wafungwa hustarehe pamoja,hawaisikii kamwe sauti ya mnyapara.

19. Wakubwa na wadogo wako huko,nao watumwa wamepata uhuru mbali na bwana zao.

20. Ya nini kumjalia nuru yule aliye taabuni;na uhai yule aliye na huzuni moyoni?

21. Mtu atamaniye kifo lakini hafi;hutafuta kifo kuliko hazina iliyofichika.

22. Mtu kama huyo atashangilia mno na kufurahi,atafurahi atakapokufa na kuzikwa!

23. Ya nini kumjalia uhai mtu ambaye njia zake zimefungwa,mtu ambaye Mungu amemwekea kizuizi?

24. Kwa maana kusononeka ndio mkate wangu,kupiga kite kwangu kunatiririka mithili ya maji.

Kusoma sura kamili Yobu 3