Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 3:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hatimaye Yobu aliamua kuongea, akailaani siku aliyozaliwa.

2. Yobu akasema:

3. “Ilaaniwe siku ile niliyozaliwa;usiku ule iliposemwa, ‘Mwana amechukuliwa mimba’

4. Siku hiyo na iwe giza!Mungu juu asijishughulishe nayo!Wala nuru yoyote isiiangaze!

5. Mauzauza na giza nene yaikumbe,mawingu mazito yaifunike.Giza la mchana liitishe!

6. Usiku huo giza nene liukumbe!Usihesabiwe katika siku za mwaka,wala usitiwe katika idadi ya siku za mwezi.

7. Naam, usiku huo uwe tasa,sauti ya furaha isiingie humo.

8. Walozi wa siku waulaani,watu stadi wa kuligutua dude Lewiyathani waulaani!

9. Nyota zake za pambazuko zififie,utamani kupata mwanga, lakini usipate,wala usione nuru ya pambazuko.

10. Maana usiku huo haukulifunga tumbo la mama,wala kuficha taabu nisizione.

11. Mbona sikufa nilipozaliwa,nikatoka tumboni na kutoweka?

12. Kwa nini mama yangu alinizaa?Kwa nini nikapata kunyonya?

Kusoma sura kamili Yobu 3