Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 21:22-31 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Je, binadamu aweza kumfunza Mungu maarifa,Mungu ambaye huwahukumu wakazi wa mbinguni?

23. “Mtu hufa katika kilele cha ufanisi wake,akiwa katika raha mustarehe na salama;

24. amejaa mafuta tele mwilini,na mifupa yake ikiwa bado na nguvu.

25. Mwingine hufa na huzuni kubwa moyoni,akiwa hajawahi kuonja lolote jema.

26. Hata hivyo, wote hufa na kuzikwa,wote hufunikwa na mabuu.

27. “Sikilizeni! Mimi nayajua mawazo yenu yote,na mipango yenu ya kunidharau.

28. Eti mwauliza, ‘Iko wapi nyumba ya mkuu?Iko wapi nyumba alimoishi mwovu?’

29. “Je, hamjawauliza wapita njia,mkakubaliana na ripoti yao?

30. Mwovu husalimishwa siku ya maafa,huokolewa siku ya ghadhabu!

31. Ni nani atakayemshutumu mtu mwovu,au atakayemlipa kwa yote aliyotenda?

Kusoma sura kamili Yobu 21