Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 21:13-25 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Huishi maisha ya fanakakisha hushuka kwa amani kuzimu.

14. Humwambia Mungu, ‘Usitusumbue!Hatutaki kujua matakwa yako.

15. Mungu Mwenye Nguvu ni nini hata tumtumikie?Tunapata faida gani tukimwomba dua?’

16. Kufanikiwa kwao si kuko mikononi mwao,wakiwa wamemweka Mungu mbali na mipango yao?

17. “Mara ngapi umepata kuona mwanga wa maisha ya mwovu umezimwa,wakapata kukumbwa na maafa,au Mungu amewahi kuwaangamiza kwa hasira yake?

18. Hata hivyo, na wapeperushwe kama majani makavu,wawe kama makapi yanayochukuliwa na dhoruba!

19. “Nyinyi mwasema, ‘Mungu amewawekea watoto waoadhabu ya watu hao waovu.’Kwa nini hawalipizi wao wenyewe, wapate kutambua!

20. Waone wao wenyewe wakiangamia;waone wenyewe ghadhabu ya Mungu mwenye nguvu.

21. Maana wakifa watajali nini juu ya wazawa wao,wakati siku zao zitakapokuwa zimefika mwisho?

22. Je, binadamu aweza kumfunza Mungu maarifa,Mungu ambaye huwahukumu wakazi wa mbinguni?

23. “Mtu hufa katika kilele cha ufanisi wake,akiwa katika raha mustarehe na salama;

24. amejaa mafuta tele mwilini,na mifupa yake ikiwa bado na nguvu.

25. Mwingine hufa na huzuni kubwa moyoni,akiwa hajawahi kuonja lolote jema.

Kusoma sura kamili Yobu 21