Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 12:9-22 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Nani kati ya viumbe hivyo,asiyejua kwamba Mwenyezi-Mungu ametenda hayo?

10. Uhai wa kila kiumbe hai umo mikononi mwake;kadhalika na pumzi ya uhai wa binadamu.

11. Je, sikio haliyapimi manenokama ulimi uonjavyo chakula?

12. Hekima iko kwa watu wazee,maarifa kwao walioishi muda mrefu.

13. Lakini hekima na uwezo ni vyake Mungu,yeye ana maarifa na ujuzi.

14. Akibomoa, hakuna awezaye kujenga upya;akimfunga mtu, hakuna awezaye kumfungua.

15. Akizuia mvua, twapata ukame;akiifungulia, nchi hupata mafuriko.

16. Yeye ana nguvu na hekima;wanaodanganywa na wanaodanganya ni wake.

17. Huwaacha washauri waende zao uchi,huwafanya waamuzi kuwa wapumbavu.

18. Huwavua wafalme vilemba vyao;na kuwafunga viunoni kamba za wafungwa;

19. Huwaacha makuhani waende uchi;na kuwaangusha wenye nguvu.

20. Huwanyanganya washauri kipawa chao cha kuongea,huwapokonya wazee hekima yao.

21. Huwamwagia wakuu aibu,huwaondolea wenye uwezo nguvu zao.

22. Huvifunua vilindi vya giza,na kuleta mwangani yaliyokuwa gizani.

Kusoma sura kamili Yobu 12