Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 12:3-12 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Mimi nami ni mwelewa kama nyinyi.Mimi si mtu duni kuliko nyinyi.Yote mliyosema kila mtu anajua.

4. Nimekuwa kichekesho kwa rafiki zangu:Mimi niliyemwomba Mungu na akanijibu;mimi niliye mwadilifu na bila lawama,nimekuwa kichekesho kwa watu.

5. Mtu anayestarehe hudharau msiba;kwake, msiba huwajia wale wanaoteleza.

6. Makao ya wanyanganyi yana amani;wenye kumchokoza Mungu wako salama,nguvu yao ni mungu wao.

7. Lakini waulize wanyama nao watakufunza;waulize ndege nao watakuambia.

8. Au iulize mimea nayo itakufundisha;sema na samaki nao watakuarifu.

9. Nani kati ya viumbe hivyo,asiyejua kwamba Mwenyezi-Mungu ametenda hayo?

10. Uhai wa kila kiumbe hai umo mikononi mwake;kadhalika na pumzi ya uhai wa binadamu.

11. Je, sikio haliyapimi manenokama ulimi uonjavyo chakula?

12. Hekima iko kwa watu wazee,maarifa kwao walioishi muda mrefu.

Kusoma sura kamili Yobu 12