Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 12:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ndipo Yobu akajibu:

2. “Sawa! Nyinyi ni watu wa hekima.Hekima itakufa wakati ule mtakapokufa.

3. Mimi nami ni mwelewa kama nyinyi.Mimi si mtu duni kuliko nyinyi.Yote mliyosema kila mtu anajua.

4. Nimekuwa kichekesho kwa rafiki zangu:Mimi niliyemwomba Mungu na akanijibu;mimi niliye mwadilifu na bila lawama,nimekuwa kichekesho kwa watu.

5. Mtu anayestarehe hudharau msiba;kwake, msiba huwajia wale wanaoteleza.

6. Makao ya wanyanganyi yana amani;wenye kumchokoza Mungu wako salama,nguvu yao ni mungu wao.

7. Lakini waulize wanyama nao watakufunza;waulize ndege nao watakuambia.

8. Au iulize mimea nayo itakufundisha;sema na samaki nao watakuarifu.

Kusoma sura kamili Yobu 12