Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 11:9-16 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Ukuu huo wapita marefu ya dunia,wapita mapana ya bahari.

10. Kama Mungu akipita,akamfunga mtu na kumhukumu,nani awezaye kumzuia?

11. Mungu anajua watu wasiofaa;akiona maovu yeye huchukua hatua.

12. “Mpumbavu hawezi kuwa na maarifa,pundamwitu ni pundamwitu tu.

13. “Yobu, ukiufanya moyo wako mnyofu,utainua mikono yako kumwomba Mungu!

14. Kama una uovu, utupilie mbali.Usikubali ubaya uwemo nyumbani mwako.

15. Hapo utajitokeza mbele ya watu bila lawama,utakuwa thabiti bila kuwa na hofu.

16. Utazisahau taabu zako zote;utazikumbuka tu kama mafuriko yaliyopita.

Kusoma sura kamili Yobu 11