Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 11:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Sofari, Mnaamathi, akamjibu Yobu:

2. “Je, wingi huu wa maneno uachwe tu bila kujibiwa?Je, mtu wa maneno mengi aonesha kuwa hana hatia?

3. Je, kuropoka kwako kutanyamazisha watu?Na kama ukidhihaki, je, hamna atakayekuaibisha?

4. Wewe wadai: ‘Ninachosema ni kweli,naam, sina lawama mbele ya Mungu.’

Kusoma sura kamili Yobu 11