Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 8:6-12 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Mimi nilisikiliza kwa makini,lakini wao hawakusema ukweli wowote.Hakuna mtu anayetubu uovu wake,wala kujiuliza; ‘Nimefanya nini?’Kila mmoja wao anashika njia yake,kama farasi akimbiliavyo moja kwa moja vitani.

7. Hata korongo anajua wakati wa kuhama;njiwa, mbayuwayu na koikoi,hufuata majira yao ya kurudi.Lakini watu wangu hawa hawajui kitujuu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.

8. Mnawezaje kusema: ‘Sisi tuna hekima,sisi tunayo sheria ya Mwenyezi-Mungu,’hali waandishi wa sheria,wameipotosha sheria yangu?

9. Wenye hekima wenu wataaibishwa;watafadhaishwa na kunaswa.Wamelikataa neno la Mwenyezi-Mungu;je, ni hekima gani hiyo waliyo nayo?

10. Kwa hiyo, wake zao nitawapa watu wengine,mashamba yao nitawapa wengine.Maana, tangu mdogo hadi mkubwa,kila mmoja ana tamaa ya faida haramu.Tangu manabii hadi makuhani,kila mmoja anatenda kwa udanganyifu.

11. Wameliponya jeraha la watu wangu juujuu,wakisema, ‘Kuna amani, kuna amani’,kumbe hakuna amani yoyote!

12. Je, waliona aibu walipotenda machukizo hayo?La hasha! Hawakuona aibu hata kidogo.Hata hawajui kuona haya.Kwa hiyo, wataanguka pamoja na wale walioanguka;nitakapowaadhibu, wataangamia.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Kusoma sura kamili Yeremia 8