Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 8:4-14 Biblia Habari Njema (BHN)

4. “Wewe Yeremia utawaambiakuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Mtu akianguka, je hainuki tena?Mtu akipotea, je, hairudii tena njia yake?

5. Mbona basi, watu hawa wameacha njia iliyo sawana kuendelea katika upotovu wao?Wanashikilia miungu yao ya uongo,na kukataa kunirudia mimi!

6. Mimi nilisikiliza kwa makini,lakini wao hawakusema ukweli wowote.Hakuna mtu anayetubu uovu wake,wala kujiuliza; ‘Nimefanya nini?’Kila mmoja wao anashika njia yake,kama farasi akimbiliavyo moja kwa moja vitani.

7. Hata korongo anajua wakati wa kuhama;njiwa, mbayuwayu na koikoi,hufuata majira yao ya kurudi.Lakini watu wangu hawa hawajui kitujuu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.

8. Mnawezaje kusema: ‘Sisi tuna hekima,sisi tunayo sheria ya Mwenyezi-Mungu,’hali waandishi wa sheria,wameipotosha sheria yangu?

9. Wenye hekima wenu wataaibishwa;watafadhaishwa na kunaswa.Wamelikataa neno la Mwenyezi-Mungu;je, ni hekima gani hiyo waliyo nayo?

10. Kwa hiyo, wake zao nitawapa watu wengine,mashamba yao nitawapa wengine.Maana, tangu mdogo hadi mkubwa,kila mmoja ana tamaa ya faida haramu.Tangu manabii hadi makuhani,kila mmoja anatenda kwa udanganyifu.

11. Wameliponya jeraha la watu wangu juujuu,wakisema, ‘Kuna amani, kuna amani’,kumbe hakuna amani yoyote!

12. Je, waliona aibu walipotenda machukizo hayo?La hasha! Hawakuona aibu hata kidogo.Hata hawajui kuona haya.Kwa hiyo, wataanguka pamoja na wale walioanguka;nitakapowaadhibu, wataangamia.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

13. “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema:Nilipotaka kukusanya chochote kutoka kwao,sikupata zabibu hata moja juu ya mzabibu,sikupata tini zozote juu ya mtini;hata majani yao yamekauka.Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.”

14. “Watu wanauliza: Kwa nini sisi tunakaa tu hapa?Kusanyikeni, tuingie katika miji yenye ngome,tukaangamie huko!Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametupangia tuangamie,ametupa maji yenye sumu tunywe,kwa kuwa tumemkosea yeye.

Kusoma sura kamili Yeremia 8