Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 50:31-38 Biblia Habari Njema (BHN)

31. “Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,napigana nawe ewe mwenye kiburi,maana siku yako ya adhabu imefika,wakati nitakapokuadhibu umewadia.

32. Mwenye kiburi atajikwaa na kuanguka,wala hapatakuwa na mtu wa kumwinua.Nitawasha moto katika miji yake,nao utateketeza kila kitu kandokando yake.”

33. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Watu wa Israeli wanakandamizwa; hali kadhalika na watu wa Yuda. Wale waliowachukua mateka wamewabana sana na wanakataa kuwaachia.

34. Lakini mimi, Mkombozi wao ni mwenye nguvu. Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina langu. Hakika nitatetea kisa chao ili nilete amani katika nchi yao, lakini taabu kwa wakazi wa Babuloni.

35. “Kifo kwa Wakaldayo,kwa wakazi wa Babulonina maofisa na wenye hekima wake!

36. Kifo kwa waaguzi,wanachotangaza ni upumbavu tu!Kifo kwa mashujaa wake,ili waangamizwe!

37. Kifo kwa farasi wake na uharibifu kwa magari yake,kifo kwa majeshi yake yote ya kukodiwa,ili wawe na woga kama wanawake!Uharibifu kwa hazina zake zoteili zipate kuporwa.

38. Ukame uyapate majiili yapate kukauka!Maana Babuloni ni nchi ya sanamu za miungu,watu ni wendawazimu juu ya vinyago vyao.

Kusoma sura kamili Yeremia 50