Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 50:24-37 Biblia Habari Njema (BHN)

24. Ewe Babuloni, nilikutegea mtego ukanaswa,wala hukujua juu yake;ulipatikana, ukakamatwa,kwa sababu ulishindana nami Mwenyezi-Mungu.

25. Nimefungua ghala yangu ya silaha,nikatoa humo silaha za ghadhabu yangu,maana mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshinina kazi ya kufanyakatika nchi ya Wakaldayo.

26. Njoni mkamshambulie kutoka kila upande;zifungueni ghala zake za chakula;mrundikieni marundo ya nafaka!Iangamizeni kabisa nchi hii;msibakize chochote!

27. Waueni askari wake hodari;waache washukie machinjoni.Ole wao, maana siku yao imewadia,wakati wao wa kuadhibiwa umefika.

28. “Sikiliza! Wakimbizi na watoro kutoka nchi ya Babuloni wanakuja kutangaza huko Siyoni jinsi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyolipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake.

29. “Waiteni wapiga mishale waishambulie Babuloni. Pelekeni kila mtu ajuaye kuvuta upinde. Uzingireni mji pasiwe na yeyote atakayetoroka. Ulipizeni kadiri ya matendo yake yote; utendeeni kama ulivyowatendea wengine, maana kwa kiburi ulinidharau mimi Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli.

30. Kwa hiyo, vijana wake watauawa katika mitaa yake, na majeshi yake yote yataangamizwa siku hiyo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

31. “Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,napigana nawe ewe mwenye kiburi,maana siku yako ya adhabu imefika,wakati nitakapokuadhibu umewadia.

32. Mwenye kiburi atajikwaa na kuanguka,wala hapatakuwa na mtu wa kumwinua.Nitawasha moto katika miji yake,nao utateketeza kila kitu kandokando yake.”

33. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Watu wa Israeli wanakandamizwa; hali kadhalika na watu wa Yuda. Wale waliowachukua mateka wamewabana sana na wanakataa kuwaachia.

34. Lakini mimi, Mkombozi wao ni mwenye nguvu. Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina langu. Hakika nitatetea kisa chao ili nilete amani katika nchi yao, lakini taabu kwa wakazi wa Babuloni.

35. “Kifo kwa Wakaldayo,kwa wakazi wa Babulonina maofisa na wenye hekima wake!

36. Kifo kwa waaguzi,wanachotangaza ni upumbavu tu!Kifo kwa mashujaa wake,ili waangamizwe!

37. Kifo kwa farasi wake na uharibifu kwa magari yake,kifo kwa majeshi yake yote ya kukodiwa,ili wawe na woga kama wanawake!Uharibifu kwa hazina zake zoteili zipate kuporwa.

Kusoma sura kamili Yeremia 50