Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 50:16-32 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Zuieni watu wasipande mbegu Babuloni,wala wasivune wakati wa mavuno.Kutokana na upanga wa udhalimu,kila mmoja atawarudia watu wakekila mmoja atakimbilia nchini mwake.

17. “Israeli ni kondoo wanaowindwa na kufukuzwa na simba. Kwanza waliangamizwa na mfalme wa Ashuru, na sasa Nebukadneza mfalme wa Babuloni, amevunjavunja mifupa yake.

18. Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Nitamwadhibu mfalme wa Babuloni na nchi yake, kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.

19. Nitawarudisha Waisraeli nchini mwao, nao watakula mavuno yatakayolimwa juu ya mlima Karmeli na Bashani na watatosheka kwa chakula kutoka milima ya Efraimu na Gileadi.

20. Siku hizo na wakati huo, uovu utatafutwa nchini Israeli, lakini hautapatikana; dhambi itatafutwa nchini Yuda, lakini haitapatikana; maana mimi nitawasamehe wale ambao nimewabakiza. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

21. “Pandeni, mwiendee nchi ya Merathaimu,nendeni kuishambulia;washambulieni wakazi wa Pekodina kuwaangamiza kabisa watu wake.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.

22. Kelele za vita zinasikika nchini,kuna uharibifu mkubwa.

23. Jinsi gani huo mji uliokuwa nyundo ya dunia nzimaunavyoangushwa chini na kuvunjika!Babuloni umekuwa kinyaamiongoni mwa mataifa!

24. Ewe Babuloni, nilikutegea mtego ukanaswa,wala hukujua juu yake;ulipatikana, ukakamatwa,kwa sababu ulishindana nami Mwenyezi-Mungu.

25. Nimefungua ghala yangu ya silaha,nikatoa humo silaha za ghadhabu yangu,maana mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshinina kazi ya kufanyakatika nchi ya Wakaldayo.

26. Njoni mkamshambulie kutoka kila upande;zifungueni ghala zake za chakula;mrundikieni marundo ya nafaka!Iangamizeni kabisa nchi hii;msibakize chochote!

27. Waueni askari wake hodari;waache washukie machinjoni.Ole wao, maana siku yao imewadia,wakati wao wa kuadhibiwa umefika.

28. “Sikiliza! Wakimbizi na watoro kutoka nchi ya Babuloni wanakuja kutangaza huko Siyoni jinsi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyolipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake.

29. “Waiteni wapiga mishale waishambulie Babuloni. Pelekeni kila mtu ajuaye kuvuta upinde. Uzingireni mji pasiwe na yeyote atakayetoroka. Ulipizeni kadiri ya matendo yake yote; utendeeni kama ulivyowatendea wengine, maana kwa kiburi ulinidharau mimi Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli.

30. Kwa hiyo, vijana wake watauawa katika mitaa yake, na majeshi yake yote yataangamizwa siku hiyo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

31. “Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,napigana nawe ewe mwenye kiburi,maana siku yako ya adhabu imefika,wakati nitakapokuadhibu umewadia.

32. Mwenye kiburi atajikwaa na kuanguka,wala hapatakuwa na mtu wa kumwinua.Nitawasha moto katika miji yake,nao utateketeza kila kitu kandokando yake.”

Kusoma sura kamili Yeremia 50