Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 47:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaushambulia mji wa Gaza:

2. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Tazama! Maji yanapanda kutoka kaskazini,nayo yatakuwa mto uliofurika;yataifunika nchi nzima na vyote vilivyomo,mji na wakazi na wanaoishi humo.Watu watalia,wakazi wote wa nchi wataomboleza.

3. Watasikia mshindo wa kwato za farasi,kelele za magari ya vita,na vishindo vya magurudumu yao.Kina baba watawasahau watoto wao,mikono yao itakuwa imelegea mno.

4. Hiyo ni siku ya kuwaangamiza Wafilisti wote,kukomesha msaada uliobakia kutoka Tiro na Sidoni.Maana Mwenyezi-Mungu anawaangamiza Wafilisti,watu waliosalia wa kisiwa cha Kaftori.

Kusoma sura kamili Yeremia 47