Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 31:4-11 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Nitakujenga upya nawe utajengeka,ewe Israeli uliye mzuri!Utazichukua tena ngoma zakoucheze kwa furaha na shangwe.

5. Utapanda tena mizabibujuu ya milima ya Samaria;wakulima watapanda mbeguna kuyafurahia mazao yake!

6. Maana siku yaja ambapo mlinzi atapiga mbiukatika vilima vya Efraimu:‘Amkeni, twende juu mpaka Siyonikwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’”

7. Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Imbeni kwa furaha kwa ajili ya Yakobo,pigeni vigelegele kwa ajili ya taifa kuu,tangazeni, shangilieni na kusema:‘Mwenyezi-Mungu na awaokoe watu wake,amewaletea ukombozi waliobaki wa Israeli!’

8. Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini,nitawakusanya kutoka miisho ya dunia.Wote watakuwapo hapo;hata vipofu na vilema,wanawake waja wazito na wanaojifungua;umati mkubwa sana utarudi hapa.

9. Watarudi wakiwa wanatoa machozi,nitawarudisha nikiwafariji;nitawapitisha kando ya vijito vya maji,katika njia iliyonyoka ambamo hawatajikwaa;maana mimi nimekuwa baba wa Israeli,Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.

10. Enyi mataifa, sikilizeni neno langu mimi Mwenyezi-Mungu,litangazeni katika nchi za mbali,semeni: ‘Aliyemtawanya Israeli, atamkusanya,atamtunza kama mchungaji atunzavyo kondoo wake.’

11. Maana mimi Mwenyezi-Mungu nimemkomboa Yakobo,nimemwokoa kutoka kwa wenye nguvu kuliko yeye.

Kusoma sura kamili Yeremia 31