Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 3:19-25 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Mwenyezi-Mungu asema,“Israeli, mimi niliwaza,laiti ningekuweka miongoni mwa wanangu,na kukupa nchi nzuri ajabu,urithi usio na kifani kati ya mataifa yote.Nilidhani ungeniita, ‘Baba Yangu’,na kamwe usingeacha kunifuata.

20. Lakini kama mke asiye mwaminifu amwachavyo mumewe,ndivyo ulivyokosa uaminifu kwangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

21. “Kelele zasikika juu ya vilima:Waisraeli wanalia na kuomboleza,kwa kuwa wamepotoka katika njia zao,wamenisahau mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.

22. Rudini, enyi watoto msio na uaminifu,mimi nitaponya utovu wenu wa uaminifu.“Nanyi mwasema: ‘Tazama, sisi tunarudi kwako,maana, wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.

23. Kweli tumedanganyika mno kuabudu huko vilimani,hakika wokovu wa Israeliwatoka kwake Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.

24. “ ‘Tangu ujana wetu, tendo hili la aibu limeangamiza kila kitu walichotolea jasho wazee wetu: Makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao.

25. Hatuna budi kujilaza chini kwa aibu, na kuiacha fedheha yetu itufunike. Tangu ujana wetu hadi leo hii, wazee wetu na sisi wenyewe tumetenda dhambi mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, wala hatukumtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’”

Kusoma sura kamili Yeremia 3