Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 18:6-21 Biblia Habari Njema (BHN)

6. “Enyi Waisraeli! Je, mimi Mwenyezi-Mungu siwezi kuwafanya nyinyi kama alivyofanya mfinyanzi huyu? Jueni kuwa kama ulivyo udongo mikononi mwa mfinyanzi, ndivyo nyinyi mlivyo mikononi mwangu.

7. Wakati wowote nitakapotoa tamko kuhusu taifa au ufalme kwamba nitalingoa na kulivunja na kuliangamiza,

8. halafu taifa hilo likageuka na kuacha uovu wake, basi, mimi nitaacha kulitendea yale mambo niliyokusudia kulitendea.

9. Hali kadhalika, wakati wowote nikitoa tamko kuhusu taifa au ufalme kwamba nitalijenga na kulistawisha,

10. kisha taifa hilo likafanya uovu mbele yangu na kukataa kunitii, basi, mimi nitaacha kulitendea mema hayo niliyokusudia kulitendea.

11. Sasa, basi, waambie watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mimi Hufinyanga jambo ovu dhidi yenu na kufanya mpango dhidi yenu. Rudini na kuacha njia zenu mbaya, mkarekebishe mienendo yenu na matendo yenu.

12. Lakini wao watasema, ‘Hiyo ni bure tu! Tutafuata mipango yetu wenyewe na kila mmoja wetu atafanya kwa kiburi kadiri ya moyo wake mwovu.’”

13. Basi, Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Yaulize mataifa yote:Nani amewahi kusikia jambo kama hili.Israeli amefanya jambo la kuchukiza mno.

14. Je, majabali ya Lebanoni hukosa theluji?Je, vijito vya maji vya milima yake hukauka?

15. Lakini watu wangu wamenisahau mimi,wanafukizia ubani miungu ya uongo.Wamejikwaa katika njia zao,katika barabara za zamani.Wanapitia vichochoroni badala ya njia kuu.

16. Wameifanya nchi yao kuwa kitisho,kitu cha kuzomewa daima.Kila mtu apitaye huko hushangaana kutikisa kichwa chake.

17. Nitawatawanya mbele ya adui,kama upepo utokao mashariki.Nitawapa kisogo badala ya kuwaonesha uso wangusiku hiyo ya kupata maafa yao.”

18. Kisha, watu wakasema: “Njoni tumfanyie Yeremia njama, maana hatukosi makuhani wa kutufundisha, wenye hekima wa kutushauri na manabii wa kututangazia ujumbe wa Mungu! Njoni tumshtaki kwa maneno yake mwenyewe, wala tusiyatilie maanani yote asemayo.”

19. Basi, mimi nikasali:Nitegee sikio ee Mwenyezi-Mungu,usikilize ombi langu.

20. Je, mtu hulipwa mabaya kwa mema?Walakini, wamenichimbia shimo.Kumbuka nilivyosimama mbele yako,nikasema mema kwa ajili yao,ili kuiepusha hasira yako mbali nao.

21. Kwa hiyo waache watoto wao wafe njaa,waache wafe vitani kwa upanga.Wake zao wawe tasa na wajane.Waume zao wafe kwa maradhi mabayana vijana wao wachinjwe kwa upanga vitani.

Kusoma sura kamili Yeremia 18