Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 17:13-17 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Ee Mwenyezi-Mungu tumaini la Israeli,wote wanaokukataa wataaibishwa;wanaokuacha wewe watatoweka,kama majina yaliyoandikwa vumbini,kwa maana wamekuacha wewe Mwenyezi-Mungu,uliye chemchemi ya maji ya uhai.

14. Uniponye, ee Mwenyezi-Mungu, nami nitapona;uniokoe, nami nitaokoka;maana, wewe ndiwe sifa yangu.

15. Tazama watu wanavyoniambia:“Jambo alilotishia Mwenyezi-Mungu liko wapi?Acha basi lije!”

16. Sikuikimbia huduma yako ya kuwa mchungajiwala sikutamani ile siku ya maafa ije.Wewe mwenyewe wajua nilichosema kwa mdomo wangu,nilichotamka wakijua waziwazi.

17. Usiwe tisho kwangu;wewe ndiwe kimbilio langu siku ya maafa.

Kusoma sura kamili Yeremia 17