Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 15:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Hata kama Mose na Samueli wangesimama mbele yangu na kunisihi, nisingewahurumia watu hawa. Waondoe kabisa mbele yangu. Waache waende zao!

2. Na wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ wewe utawajibu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Waliopangiwa kufa kwa maradhi, watakufa kwa maradhi;waliopangiwa kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga;waliopangiwa kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa;na waliopangiwa kuwa mateka, watatekwa mateka.

3. Mimi Mwenyezi-Mungu nimeamua kuwaletea aina nne za maangamizi: Vita itakayowaua, mbwa watakaowararua; ndege wa angani watakaowadonoa na wanyama wa porini watakaowatafuna na kuwamaliza.

4. Nitawafanya kuwa kitu cha kutisha kwa falme zote za dunia, kwa sababu ya mambo ambayo Manase mwana wa Hezekia, aliyafanya huko Yerusalemu, alipokuwa mfalme wa Yuda.

5. “Ni nani atakayewahurumia, enyi watu wa Yerusalemu?Ni nani atakayeomboleza juu yenu?Nani atasimama kuuliza habari zenu?

6. Nyinyi mmenikataa mimi, nasema mimi Mwenyezi-Mungu;nyinyi mmeniacha mkarudi nyuma.Hivyo nimenyosha mkono kuwaangamiza,kwa kuwa nimechoka kuwahurumia.

7. Nimewapepeta kwa chombo cha kupuria,katika kila mji nchini;nimewaangamiza watu wangu,kwa kuwaulia mbali watoto wao,lakini hawakuacha njia zao.

8. Wajane wao wamekuwa wengikuliko mchanga wa bahari.Kina mama wa watoto walio vijananimewaletea mwangamizi mchana.Nimesababisha uchungu na vitishoviwapate kwa ghafla.

9. Mama aliyesifika kuwa na watoto saba;sasa ghafla hana kitu.Ametoa pumzi yake ya mwisho,jua lake limetua kukiwa bado mchana;ameaibishwa na kufedheheshwa.Na wale waliobaki hai nitawaachawauawe kwa upanga na maadui zao.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

10. Ole wangu, mama yangu, kwamba ulinizaa! Mimi nimekuwa mtu wa ubishi na ugomvi nchini pote! Sijapata kukopesha mtu wala kukopeshwa na mtu, lakini kila mtu ananiapiza.

11. Haya basi, ee Mwenyezi-Mungu, acha laana hizo nizipate kama sijakutumikia vema na kama sikukusihi kwa ajili ya maadui zangu wakati walipokuwa katika taabu na shida!

12. Je, mtu aweza kuvunja chuma, chuma kitokacho kaskazini, au shaba?

Kusoma sura kamili Yeremia 15