Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 14:17-22 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Hivi ndivyo utakavyowaambia:Laiti macho yangetoa machozi kutwa kucha,wala yasikome kububujika,maana, watu wangu wamejeruhiwa vibaya,wamepata pigo kubwa sana.

18. Nikienda nje mashambani,naiona miili ya waliouawa vitani;nikiingia ndani ya mji,naona tu waliokufa kwa njaa!Manabii na makuhani wanashughulikia mambo yao nchini,wala hawajui wanalofanya.”

19. Ee Mwenyezi-Mungu, je, umemkataa Yuda kabisa?Je, moyo wako umechukizwa na Siyoni?Kwa nini umetupiga vibaya,hata hatuwezi kupona tena?Tulitazamia amani, lakini hatukupata jema lolote;tulitazamia wakati wa kuponywa, badala yake tukapata vitisho.

20. Tunakiri uovu wetu, ee Mwenyezi-Mungu,tunakiri uovu wa wazee wetu,maana, tumekukosea wewe.

21. Usitutupe, kwa heshima ya jina lako;usikidharau kiti chako cha enzi kitukufu.Ukumbuke agano ulilofanya nasi, wala usilivunje.

22. Je miungu ya uongo ya mataifayaweza kuleta mvua?Au, je, mbingu zaweza kutoa manyunyu?Je, si wewe ee Mwenyezi-Mungu uliye Mungu wetu?Tunakuwekea wewe tumaini letu,maana wewe unayafanya haya yote.

Kusoma sura kamili Yeremia 14