Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 14:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia kuhusu ule ukame:

2. “Watu wa Yuda wanaomboleza,na malango yao yanalegea.Watu wake wanaomboleza udongonina kilio cha Yerusalemu kinapanda juu.

3. Wakuu wake wanawatuma watumishi wao maji;watumishi wanakwenda visimani,lakini maji hawapati;wanarudi na vyombo vitupu.Kwa aibu na fadhaa wanafunika vichwa vyao.

4. Wakulima wanahuzunika na kufunika vichwa vyaokwa kuona jinsi ardhi ilivyonyauka.

5. Hata kulungu porini anamwacha mtoto wake mchanga,kwa sababu hakuna nyasi.

6. Pundamwitu wanasimama juu ya vilele vikavu,wanatweta kwa kukosa hewa kama mbweha;macho yao yanafifia kwa kukosa chakula.

7. “Nao watu wanasema:Ingawa dhambi zetu zashuhudia dhidi yetu,utusaidie ee Mwenyezi-Mungu kwa heshima ya jina lako.Maasi yetu ni mengi,tumetenda dhambi dhidi yako.

8. Ewe uliye tumaini la Israeli,mwokozi wetu wakati wa taabu,utakuwaje kama mgeni nchini mwetu,kama msafiri alalaye usiku mmoja?

9. Utakuwaje kama mtu uliyechanganyikiwa,kama shujaa asiyeweza kusaidia mtu?Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu, u pamoja nasi;sisi twaitwa kwa jina lako, usituache.”

Kusoma sura kamili Yeremia 14